Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MHANDISI RAMADHANI MTINDASI
MHANDISI RAMADHANI MTINDASI
Mkurugenzi Mtendaji
KAribu SUWASA-Ninayofuraha kukukaribisha katika tovuti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA). To...

Habari Mpya
MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA  VYANZO VYA  MAJI VYA MAMLAKA YA MAJI SINGIDA.
MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VYANZO VYA MAJI VYA MAMLAKA YA MAJI SINGIDA.
19-07-2026 15:59:40
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe akiambatana na Katibu Tawala Bi. Naima Chondo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikishirikiana na Menejimenti ya SUWASA tarehe 17.07.2026  imefanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji vya Mwankoko, Uhasibu, Utemini na Irao kwa lengo la kugua hali ya uzalishaji wa maji wa sasa na kujionea  maboresho ya yanayo endelea kufanywa na SUWASA katika chanzo hivyo.Katika ziara hiyo Mhe. Mkuu wa Wilaya na Kamati yake wameweza kuona jitihada za muda mfupi na wa kati zinazo endelea kufanywa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) pamoja na Serikali katika kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa na kupatikana kwa wananchi.  Jitihada hizo ni pamoja na kuchimba na kufukia bomba, ufungaji wa Pampu na kuweka miundombinu ya  umeme katika visima viwili vya mwankoko ambavyo kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha lita 133,000 kwa saa na kingine lita 94,000 kwa saa, pia Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kutembelea visima vingine viwili vya Uhasibu na Utemini ambavyo viko katika uboreshaji visima hivi kwa pamojq vina uwezo wa kuzalisha lita 40,000 kwa saa.Kukamilika kazi ya kuunganishwa kwa kisima hivi vyote kutaongeza upatikanaji wa maji katika mfumo wa uzalishai wa SUWASA kutoka asilimia 40 ya sasa hadi asilimia 59.Aidha  Mhe. Godwin Gondwe ameipongeza Menejimenti ya SUWASA ikiongozwa na Mhandisi Ramadhani Mtindasi kwa kuendelea kufanya jitihada za kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi na amesis...
KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA SINGIDA NA MADIWANI WA MANISPAA SINGIDA WAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MABORESHO YA CHANZO CHA MAJI MWANKOKO
KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA SINGIDA NA MADIWANI WA MANISPAA SINGIDA WAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAB ..
14-07-2026 09:23:34
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe. Lucia Mwiru pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Singida wakiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Geofrey Mdamu wakiwa na Menejimenti ya SUWASA jana tarehe 08.07.2026 imefanya ziara ya kukagua maboresho ya yanayo endelea kufanywa na SUWASA katika chanzo cha maji cha Mwankoko.Katika ziara hiyo Kamati na Madiwani waliweza kuona jitihada za muda mfupi na wa kati zinazo endelea kufanywa na Mamlaka pamoja Serikali katika kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi. Jitihada hizo ni pamoja na kuchimba na kuweka miundombinu ya visima viwili vya mwankoko ambapo kimoja kina uwezo wa kuzalisha lita 133,000 kwa saa na kingine lita 90,000 kwa saa sambambana visima vinavyohitaji maboresho vya Uhasibu na Utemini visima hivi vina uwezo wa kuzalisha lita 30,000 kwa saa.Visima hivyo vimechimbwa na kukamilika kati ya hivyo kimoja bomba zimelazwa kinasubiri kufungwa pump kwaajili ya kusukuma maji kukamilika kuunganishwa kwa kisima hiki kutasaidia kuondoa nakisi iliyopo kutoka asilimia 40 ya sasa hadi asilimia 59.Aidha kamati na waheshimiwa Madiwani wamepongeza Menejimenti ya SUWASA ikiongozwa na Mhandisi Ramadhani Mtindasi kwa kuwaalika ili kuja kujionea Miradi inayoendelea na kumsihi aendelee kushirikiana kufikia malengo ya kuipata Singida yetu yenye neema ya maji na kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi.Aidha nae Mh. Mbunge wa Singida Mjini Mhe. Yagi Kiaratu ameipongeza SUWASA kwa ushirikiano na...
MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA SINGIDA (SUWASA) ATEMBELEA KANDA YA IGUGUNO, SEPUKA NA IRISYA KUJUA HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI.
MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA SINGIDA (SUWASA) ATEMBELEA KANDA Y ..
03-07-2026 23:08:18
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo  tarehe 03.07.2026 akiongozana na watumishi walio chini yake ametembelea  Kanda ya IGUGUNO, SEPUKA na IRISYA ambayo pia ni sehemu ya eneo la huduma la SUWASA.Katika ziara hiyo Mha. Ramadhani Mtindasi ametembelea Matanki ya Kuhifadhia maji ya Sepuka,Irisya, Mwanangiri na Iguseru pia ametembelea vyanzo vya maji vya Sepuka, Irisya, na Iguguno .Lengo la ziara hiyo ni kujionea hali ya utoaji huduma ya maji safi katika maeneo hayo pamoja na hali ya vyanzo vinavyo hudumia maeneo hayo, ziara hiyo pia ilikuwa ina angalia namna bora ya  kuboresha vyanzo hivyo  na kuongeza uzalishaji lakini pia kuona namna ya kupunguza nakisi iliyo kati ya uzalishaji na mahitaji. Kwa sasa SUWASA  katika kanda ya Iguguno, Sepuka na Irisya inauwezo wa kuzalisha maji na kuweza kuhudumia asilimia 60 ya mahitaji.Aidha Mkurugenzi Mtindasi  amepokea taarifa ya utendaji kazi wa Kanda kutoka kwa Meneja wa SUWASA Kanda ya Iguguno  Bw. Kassimu Jumbe. Pia Bwana Kassimu Jumbe alieleza changamoto ya kanda hiyo ikiwepo ya kukabiliwa na kuwa na mtandao mdogo wa mabomba ya Usambazaji.Mhandisi Mtindasi ameahidi kufanyia kazi changamoto hizo kwa  kushirikiana na Menejimenti yake na kuweza kuboresha huduma ya MajiSafi katika Kanda hiyo kutoka asilimia 60 ya sasa na kufikia lengo lililo wekwa na Serikali la utoaji huduma ya maji mijini na vijijini.Aidha Mha. Mtindasi...