Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MKURUGENZI MTENDAJI SUWASA ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MKOANI SINGIDA


Mkurugenzi Mtendaji SUWASA Mha. Ramadhani Mtindasi akiambatana na watumishi walio chini yake leo Tarehe 19 Julai 2026 ameshiriki katika mapokezi rasmi ya Mwenge wa  Uhuru Mkoa wa Singida katika viwanja vya shule ya Msingi Mwasauya iliyopo Ngamu Halmashauri ya Wilaya Singida.


Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi pamoja na kukagua Mradi wa uboreshaji wa Huduma ya MajiSafi eneo la Mtipa Mashariki Manuspaa ya Singida.


SUWASA tuna tekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026: Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo.