Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA SINGIDA (SUWASA) ATEMBELEA KANDA YA IGUGUNO, SEPUKA NA IRISYA KUJUA HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo  tarehe 03.07.2026 akiongozana na watumishi walio chini yake ametembelea  Kanda ya IGUGUNO, SEPUKA na IRISYA ambayo pia ni sehemu ya eneo la huduma la SUWASA.


Katika ziara hiyo Mha. Ramadhani Mtindasi ametembelea Matanki ya Kuhifadhia maji ya Sepuka,Irisya, Mwanangiri na Iguseru pia ametembelea vyanzo vya maji vya Sepuka, Irisya, na Iguguno .


Lengo la ziara hiyo ni kujionea hali ya utoaji huduma ya maji safi katika maeneo hayo pamoja na hali ya vyanzo vinavyo hudumia maeneo hayo, ziara hiyo pia ilikuwa ina angalia namna bora ya  kuboresha vyanzo hivyo  na kuongeza uzalishaji lakini pia kuona namna ya kupunguza nakisi iliyo kati ya uzalishaji na mahitaji. Kwa sasa SUWASA  katika kanda ya Iguguno, Sepuka na Irisya inauwezo wa kuzalisha maji na kuweza kuhudumia asilimia 60 ya mahitaji.


Aidha Mkurugenzi Mtindasi  amepokea taarifa ya utendaji kazi wa Kanda kutoka kwa Meneja wa SUWASA Kanda ya Iguguno  Bw. Kassimu Jumbe.


 Pia Bwana Kassimu Jumbe alieleza changamoto ya kanda hiyo ikiwepo ya kukabiliwa na kuwa na mtandao mdogo wa mabomba ya Usambazaji.


Mhandisi Mtindasi ameahidi kufanyia kazi changamoto hizo kwa  kushirikiana na Menejimenti yake na kuweza kuboresha huduma ya MajiSafi katika Kanda hiyo kutoka asilimia 60 ya sasa na kufikia lengo lililo wekwa na Serikali la utoaji huduma ya maji mijini na vijijini.


Aidha Mha. Mtindasi amewasisitiza watumishi wa Kanda  hizo kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha huduma ya maji  sambamba na kuongeza idadi ya wateja ili kuongeza mapato ambayo yatatumika kuboresha huduma ya MajiSafi katika maeneo hayo.


##kazinaututunasongambele.