Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MKUU WA WILAYA YA SINGIDA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VYANZO VYA MAJI VYA MAMLAKA YA MAJI SINGIDA.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe akiambatana na Katibu Tawala Bi. Naima Chondo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikishirikiana na Menejimenti ya SUWASA tarehe 17.07.2026  imefanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji vya Mwankoko, Uhasibu, Utemini na Irao kwa lengo la kugua hali ya uzalishaji wa maji wa sasa na kujionea  maboresho ya yanayo endelea kufanywa na SUWASA katika chanzo hivyo.


Katika ziara hiyo Mhe. Mkuu wa Wilaya na Kamati yake wameweza kuona jitihada za muda mfupi na wa kati zinazo endelea kufanywa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) pamoja na Serikali katika kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa na kupatikana kwa wananchi.  Jitihada hizo ni pamoja na kuchimba na kufukia bomba, ufungaji wa Pampu na kuweka miundombinu ya  umeme katika visima viwili vya mwankoko ambavyo kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha lita 133,000 kwa saa na kingine lita 94,000 kwa saa, pia Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kutembelea visima vingine viwili vya Uhasibu na Utemini ambavyo viko katika uboreshaji visima hivi kwa pamojq vina uwezo wa kuzalisha lita 40,000 kwa saa.


Kukamilika kazi ya kuunganishwa kwa kisima hivi vyote kutaongeza upatikanaji wa maji katika mfumo wa uzalishai wa SUWASA kutoka asilimia 40 ya sasa hadi asilimia 59.


Aidha  Mhe. Godwin Gondwe ameipongeza Menejimenti ya SUWASA ikiongozwa na Mhandisi Ramadhani Mtindasi kwa kuendelea kufanya jitihada za kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi na amesisitiza kuwa kwa kiasi cha maji kinacho zalishwa kigawiwe kwa uwiano sawa kwa kufuata ratiba iliyo na wananchi watangaziwe na waifahamu ratiba ya mgawo huo ili kupunguza malalamiko.


Aidha katika ziara hiyo nae Katibu Tawala Bi. Naima Chondo na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama waliweza kutoa mapendekezo na maoni mbalimbali ya uboreshaji huduma ya maji katika Manispaa ya Singida  na kushukuru kwa jitihada zinazoendelea katika maboresho ya huduma ya MajiSafi.


Aidha Mkurugenzi Mtendaji SUWASA Mha. Ramadhani Mtindasi kwa kushirikiana na Menejimenti  ya SUWASA amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutenga muda wake adimu na kuweza kupita na kujionea hali ya upatikanaji wa maji na jitihada zinazofanywa na SUWASA katika kuboresha huduma na ameahidi kuyafanya kazi kwa nguvu na bidii kubwa mapendekezo yote yaliyo tolewa na  ameomba ushirikiano ili kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi wa Singida. 

##kazinaututunasongambele.