Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA YATOA ELIMU JUU YA MATUMIZI YA MAJI KATIKA MRADI MPYA WA MAJI ENEO LA MTIPA MASHARIKI.


SUWASA YATOA ELIMU JUU YA MATUMIZI YA MAJI KATIKA MRADI  MPYA WA MAJI ENEO LA MTIPA MASHARIKI.


Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA)jana  tarehe  29.07.2026 imetoa elimu kwa wananchi wa Mtipa Mashariki kata ya Mtipa juu ya matumizi ya maji katika Mradi mpya wa maji ulizinduliwa.


Elimu  hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma  Bw. Maiki Simoni Ndahani aliyeongozana na watumishi wengine ambapo amewaeleza wananchi hao kuwa Mradi  wa maji  umeanza kufanya kazi hivyo wanatakiwa kuendelea kuutunza vizuri ili uwe endelevu.


Aidha ametolea ufafanuzi juu ya bei ya maji kwa ndoo moja ya lita 20 yenye ujazo wa kawaida katika magati  ni TZS 35 ambapo kwa  ndoo 3 ni TZS 100. amewaeleza kuwa gharama hizo wanazochangia kwa kulipia maji ndizo zinazotumika kununua madawa,umeme na vifaa vya matengenezo.


Pia amesisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji, kuepuka kuchunga mifugo karibu na chanzo na kulinda miundombinu ya maji ikiwemo  mabomba ili kuepuka upotevu wa maji.


Bw. Maiki Ndahani amewashukuru wananchi waliofika na kuwaagiza waendelee kupeana taarifa zaidi na kuelimishana juu ya matumizi ya maji , utunzaji wa Mradi huo na miundombinu yake na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.

###kazinaututunasongambele.