KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA SINGIDA NA MADIWANI WA MANISPAA SINGIDA WAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MABORESHO YA CHANZO CHA MAJI MWANKOKO
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe. Lucia Mwiru pamoja na Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Singida wakiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Geofrey Mdamu wakiwa na Menejimenti ya SUWASA jana tarehe 08.07.2026 imefanya ziara ya kukagua maboresho ya yanayo endelea kufanywa na SUWASA katika chanzo cha maji cha Mwankoko.
Katika ziara hiyo Kamati na Madiwani waliweza kuona jitihada za muda mfupi na wa kati zinazo endelea kufanywa na Mamlaka pamoja Serikali katika kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi. Jitihada hizo ni pamoja na kuchimba na kuweka miundombinu ya visima viwili vya mwankoko ambapo kimoja kina uwezo wa kuzalisha lita 133,000 kwa saa na kingine lita 90,000 kwa saa sambambana visima vinavyohitaji maboresho vya Uhasibu na Utemini visima hivi vina uwezo wa kuzalisha lita 30,000 kwa saa.
Visima hivyo vimechimbwa na kukamilika kati ya hivyo kimoja bomba zimelazwa kinasubiri kufungwa pump kwaajili ya kusukuma maji kukamilika kuunganishwa kwa kisima hiki kutasaidia kuondoa nakisi iliyopo kutoka asilimia 40 ya sasa hadi asilimia 59.
Aidha kamati na waheshimiwa Madiwani wamepongeza Menejimenti ya SUWASA ikiongozwa na Mhandisi Ramadhani Mtindasi kwa kuwaalika ili kuja kujionea Miradi inayoendelea na kumsihi aendelee kushirikiana kufikia malengo ya kuipata Singida yetu yenye neema ya maji na kupunguza changamoto ya maji kwa wananchi.
Aidha nae Mh. Mbunge wa Singida Mjini Mhe. Yagi Kiaratu ameipongeza SUWASA kwa ushirikiano na kushauri SUWASA kuzidisha utafiti na utambuzi wa kutafuta maji na kutambua mtandao wa maji uliopo ili kuboresha ufanisi katika utendaji kazi wa Mamlaka
Pia Mhe. Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Singida Mr. Mdama amewataka wataalamu SUWASA na watumishi kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha tatizo la maji Manispaa ya Singida linapata suluhu. Pia amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa kwa kuboresha huduma ya maji maeneo ya pembeni ya mji ikiwemo Mtamaa, Unyianga, Mtisi, Uhamaka na Unyamikumbi.
Aidha katika ziara hiyo nao waheshimiwa Madiwani waliweza kutoa mapendekezo na maoni mbalimbali ya uboreshaji huduma ya maji katika Manispaa ya Singida ikiwemo kuitaka SUWASA kufuata ratiba ya mgawo wa maji, suala la maunganisho mapya, ufungaji wa mita za malipo ya kabla , uwekaji na uboreshaji wa magati ya kuchotea maji.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji SUWASA Mha. Ramadhani Mtindasi kwa kushirikiana na Menejimenti ya SUWASA ameahidi kuyafanyia kazi maoni na mapendekezo yote ambayo kamati na Waheshimiwa Madiwani imeshauri kwaajili ya kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa kwa wananchi.