Habari
News
SUWASA STAFF PARTICIPATE IN e-Utendaji SYSTEM TRAINING
WATUMISHI WA SUWASA WASHIRIKI MAFUNZO YA MFUMO WA e-Utendaji
Posted on: Jul 18, 2025 Imetengenezwa: Jul 18, 2025
Staff from the Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) participated in training on the e-Utendaji Management System (PEPMIS) held on June 16, 2025, at the Singida Regional Commissioner’s Office hall.
The training involved leaders including heads of institutions, heads of departments from public institutions, district councils within the Singida region, the Regional Commissioner’s Office, teachers, and the regional hospital.
The session was conducted by experts from the President’s Office – Public Service Management and Good Governance, led by Assistant Director of the Government Performance and Contracts Department, Elizabeth Makyao, and Senior Officer Mr. Aidan Lucas.
Ms. Elizabeth stated that the objective of the training was to help leaders identify and resolve existing challenges, and to improve implementation and supervision of the system to ensure that public servants receive their rightful benefits, such as promotions.
Let me know if you'd like a shorter summary or a version tailored for of
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) wameshiriki mafunzo ya Mfumo wa e- Utendaji yaliyofanyika tarehe 16 Juni 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida. Mafunzo hayo ya e-Utendaji (PEPMIS) yalihusisha Viongozi ambao ni Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Vitengo kutoka Taasisi za Umma, Halmashauri za mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Walimu na Hospitali ya Mkoa. Mafunzo hayo yalitolewa na Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala bora,ambao ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mikataba na Utendaji Serikalini Elizabeth Makyao na Afisa Mwandamizi Ndg. Aidan Lucas
Bi. Elizabeth amesema lengo la kutoa mafunzo hayo kwa Viongozi ni kutambua na kutatua changamoto zilizopo pamoja na kuboresha Utekelezaji na usimamizi wa Mfumo huo ili kuhakikisha watumishi wanapata stahiki zao kama kupanda madaraja.