Habari
News
SUWASA ENTERS TOP TEN AMONG 84 WATER AUTHORITIES BEST IN PROVIDING INFORMATION IN THE COUNTRY
SUWASA YAINGIA KUMI BORA KATI YA MAMLAKA ZA MAJI 84 ZILIZO BORA KATIKA UTOAJI WA TAARIFA NCHINI
Posted on: Jun 24, 2024 Imetengenezwa: Jun 24, 2024
Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) has entered the list of the top 10 authorities that performs well in informing the Public, among the total of 84 Water Authorities in the country where SUWASA has ranked 9th.
This has been said by the Director of the Department of Information and Chief Government Spokesperson Thomas Makoba at the Conference of the Development of the Information Sector and the Government's Information Officers Annual Conference that started on 18-22 June 2024 where the Guest of Honour was the President of the United Republic of Tanzania Hon. Dr. Samia Suluhu Hassan.
The Hon.President has directed the Information Officers to observe the ethics of journalism, to avoid writing inflammatory news and instead to explain the good things done by the Government of Tanzania.
Dr. Samia has said that she supports the freedom of the media as it is the basis for strengthening democracy in the country.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeingia katika orodha ya Mamlaka kumi bora zinazofanya vizuri katika utoaji wa taarifa kati ya jumla ya Mamlaka za Maji 84 nchini ambapo SUWASA imeshika nafasi ya 9. Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Thomas Makoba katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari na kikao kazi lililoanza tarehe 18-22 Juni 2024 ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan. Mhe. Rais amewaelekeza Maafisa habari kuzingatia Maadili ya uandishi wa habari, kuepuka kuandika habari zenye kuleta uchochezi na badala yake kueleza yale mazuri yanayofanywa na Serikali ya Tanzania. Dkt. Samia amesema anaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari kwani ni Msingi wa kuimarisha Demokrasia nchini.