Habari

News

SUWASA PARTICIPATE IN THE 41st GRADUATION CEREMONY OF THE PUBLIC SERVICE COLLEGE

SUWASA YASHIRIKI MAHAFALI YA 41 YA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA

Posted on: Jun 5, 2025 Imetengenezwa: Jun 5, 2025

The Singida Urban Water and Sanitation Authority (SUWASA) participated in the 41st Graduation Ceremony of the Public Service College, which was held at the Social Hall of the Catholic Church, in Singida Municipality.

The Guest of Honor at the ceremony, Hon. George Boniface Simbachawene (MP), Minister in the President’s Office for Public Service Management and Good Governance, congratulated the Principal of the Public Service College, Dr. Ernest Mabonesho, along with the management team for the good work they are doing, as well as the graduates for their excellent academic performance.

He also commended the college leadership for the various research efforts being undertaken, which help address different challenges in the public service sector. He urged the college to continue offering professional training to public servants both before and during their employment, emphasizing that human resources are crucial and such training helps build the capacity of employees to improve accountability and keep up with the times.

Hon. Simbachawene encouraged the graduates to uphold the public service ethics they have learned and to demonstrate a positive impact in their communities and workplaces, especially those who are already employed.

A total of 1,330 students graduated with certificates and diplomas in various fields.
#kaziiendelee

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeshiriki katika Mahafali ya 41 ya Chuo cha Utumishi wa Umma, iliyofanyika katika Ukumbi wa Social wa Kanisa la kikatoliki, Manispaa ya Singida.

Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, Waziri wa Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Boniface Simbachawene (Mb) amempongeza Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dr. Ernest Mabonesho pamoja na Menejimenti kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya, pamoja na wahitimu kwa kufanya vizuri katika masomo yao. Aidha amepongeza Uongozi wa Chuo kwa tafiti mbalimbali wanazofanya, ambazo husaidia kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi, amehimiza chuo kuendelea kutoa mafunzo ya kiutumishi kwa watumishi wa Umma, kabla ya ajira na wakati wa ajira, kwani Rasilimali watu ni muhimu sana, na mafunzo hayo husaidia kujenga uwezo wa watumishi ili kuboresha uwajibikaji na kwenda na wakati.

Mhe. Simbachawene amewataka wahitimu kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma waliyoyapata, na kuonyesha tofauti katika jamii na katika maeneo yao ya kazi kwa wale walioajiriwa. Jumla ya wanafunzi 1330 wamehitimu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada za fani mbalimbali. #kaziiendelee

Anwani
Address
  • Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida Singida Water Supply and Environmental Sanitation Authority
  • P.O. Box 174,
    Singida.
  • +2552502122, 0800710038
  • info@suwasa.or.tz
Tovuti Mashuhuri
Related Links
Idadi ya Wageni
Visitors Counter
  • Today Leo 17
  • Yesterday Jana 1,636
  • This Week Wiki hii 2,911
  • This Month Mwezi huu 29,381
  • All Days Siku Zote 341,232
Hakimiliki ©2023 SUWASA. Haki zote zimehifadhiwa.