Habari

News

SUWASA PROVIDES WATER SERVICE EDUCATION IN UNYANGA

SUWASA YATOA ELIMU YA HUDUMA YA MAJI UNYIANGA

Posted on: Jul 21, 2025 Imetengenezwa: Jul 21, 2025

The Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) has provided water service education to residents of Unyianga B during a meeting held at the Office of the Ward Executive Officer in Unyianga.

The education was delivered by SUWASA officials, Environmental Engineer Kassim Abdallah and Public Relations and Communications Officer Neema Lulandala, in collaboration with Hydrologist Fredy Salehe Nzingula from the Central Water Basin Board.

While outlining SUWASA's plans for the ward, they explained that SUWASA is continuing with a service improvement project in the Unyianga A area, where a borehole has been drilled, a 10,000-liter water tank tower has been constructed, and a water fetching kiosk has been built. Additionally, groundwater surveys under the Miji 28 Water Supply Project are ongoing.

They further explained that SUWASA intends to improve the existing borehole located at the Mwankoko water source conservation area, which is expected to also serve the Unyianga B area.

Clarification was also provided regarding groundwater availability, required water quality standards, and the amount of water needed from a borehole as per the Ministry of Water guidelines, all of which are considered when developing these wells.

Engineer Kassim clarified that the surface water observed in that area has already been studied and found to be insufficient to support borehole drilling. Therefore, residents were urged to remain patient as SUWASA continues its work on projects aimed at resolving the water service challenges in Unyianga Ward during the 2025/2026 financial year.

Meanwhile, Mr. Nzingula provided education on groundwater source exploration, water quality management, conservation of those sources, and the issuance of permits for drilling deep wells.

The Unyianga Ward Executive Officer, Andrew Mchomvu, expressed his deep gratitude to SUWASA for the education provided, noting that it helped answer many questions from the residents and brought about shared understanding.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imetoa elimu ya huduma ya maji Unyianga B, katika Mkutano uliofanyika eneo la Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Unyianga.

Elimu hiyo imetolewa na Maafisa wa SUWASA Mhandisi Mazingira Kassim Abdallah na Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Neema Lulandala wakishirikiana na Afisa kutoka Bodi ya Maji Bonde la kati Mhaidrolojia Fredy Salehe Nzingula Wakieleza mipango ya SUWASA katika kata hiyo

Wameeleza kuwa SUWASA inaendelea na mradi wa Uboreshaji huduma eneo la Unyanga A, ambapo imechimba kisima na imejenga mnara wa Tanki la lita 10000 na kioski cha kuchotea maji. Aidha utafiti wa maji chini ya Ardhi kupitia Mradi wa Majisafi wa miji 28 unaendelea.

Halikadhalika wameeleza kuwa SUWASA inatarajia kuboresha kisima kilichopo eneo la hifadhi ya chanzo cha Majisafi cha Mwankoko ambacho kinatarajiwa kusaidia pia kuhudumia eneo hilo la Unyanga B

Aidha ufafanuzi umetolewa kuhusiana na upatikanaji wa maji chini ya ardhi, viwango stahiki vya Ubora wa maji na kiasi cha maji yanayotakiwa katika kisima kwa mujibu wa Wizara ya Maji, ambavyo vyote huzingatiwa katika upatikanaji wa visima hivyo.

Mhandisi Kassim amefafanua kwamba maji yanayoonekana juu ya ardhi katika eneo hilo yameshafanyiwa utafiti na kuonekana kuwa hayawezi kukidhi mahitaji ya uchimbaji wa kisima. Hivyo wananchi wameombwa kuvuta subira kwani SUWASA ipo kazini na inaendelea na miradi ambayo itaondoa changamoto ya huduma ya maji kata ya Unyianga katika mwaka huu wa fedha 2025/2026

Naye Nzingula ametoa elimu ya utafiti wa vyanzo vya maji chini ya ardhi, usimamizi wa ubora wa maji, utunzaji wa vyanzo hivyo pamoja na utoaji wa vibali vya kuchimba visima virefu. Mtendaji wa Kata ya Unyianga Andrew Mchomvu ameishukuru sana SUWASA kwa elimu iliyotolewa kwani imesaidia kujibu maswali mengi kutoka kwa wananchi na kuleta uelewa wa pamoja.

Anwani
Address
  • Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida Singida Water Supply and Environmental Sanitation Authority
  • P.O. Box 174,
    Singida.
  • +2552502122, 0800710038
  • info@suwasa.or.tz
Tovuti Mashuhuri
Related Links
Idadi ya Wageni
Visitors Counter
  • Today Leo 943
  • Yesterday Jana 1,636
  • This Week Wiki hii 3,836
  • This Month Mwezi huu 30,306
  • All Days Siku Zote 342,157
Hakimiliki ©2023 SUWASA. Haki zote zimehifadhiwa.