Habari
News
SUWASA PARTICIPATES IN THE SINGIDA REGIONAL NUTRITION COMMITTEE MEETING
SUWASA IMESHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA LISHE YA MKOA WA SINGIDA
Posted on: Sep 15, 2025 Imetengenezwa: Sep 15, 2025
Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) participated in a preparatory meeting of the Singida Regional Nutrition Committee, held at the office of the Singida Regional Commissioner.
The meeting involved officials and committee members, with the aim of discussing various steps for implementing the resolutions of the meeting held on May 12, 2025, including the use of the GoTHOMIS system for managing healthcare services, the installation of machines to add nutrients to maize flour to combat stunting, malnutrition, underweight, anemia in children under 5 years, the distribution of vitamin D drops to pregnant women, and the allocation of nutrition funds.
The members received a report on the state of nutrition in the region and the implementation of the nutrition contract for the period from July 2024 to March 2025.
The Chairperson of the meeting, Acting Regional Administrative Secretary of Singida, Mr. Pancras Stephen, directed all directors of Singida district councils and nutrition officers to ensure they provide sufficient education on the importance of these nutrients, in order to avoid the challenges of misconceptions that hinder the success of this initiative.
Nutrition officers were instructed to complete the implementation of all resolutions effectively and on time, to achieve good results and eliminate the problems caused by the lack of these nutrients.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeshiriki kikao cha maandalizi ya Kamati ya lishe ya Mkoa wa Singida kilichofanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Kikao hicho kimehusisha watendaji na wana Kamati, lengo likiwa ni kujadili hatua mbalimbali za utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichofanyika tarehe 12 Mei 2025, ikiwa ni pamoja na Utumiaji wa mfumo wa GoTHOMIS wa kusimamia utoaji wa huduma za afya, ufungaji wa mashine za kuongeza virutubishi katika unga wa mahindi kwa ajili ya kupambana na ukondefu, udumavu, uzito pungufu, upungufu wa damu . kwa watoto chini ya miaka 5, ugawaji wa matone ya vitamin D kwa wakina mama wajawazitopamoja na utengaji wa fedha za Lishe.
Wajumbe walipokea Taarifa ya hali ya lishe ya Mkoa na Utekelezaji wa Mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025.
Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw. Pancras Stephen ameelekeza Wakurugenzi wote wa halmashauri za Mkoa wa Singida pamoja na Maafisa Lishe, kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa virutubishi hivyo, ili kuepukana na changamoto ya imani potofu, inazokwamisha ufanisi wa zoezi hilo.
Maafisa Lishe wameelekezwa kukamilisha utekelezaji wa maazimio yote kwa ufanisi mkubwa na kwa wakati, ili kupata matokeo mazuri na kuondoa matatizo yanayosababishwa na ukosefu wa virutubishi hivyo.