Habari
News
SUWASA PROVIDED ENVIROMENTAL CONSERVATION EDUCATION
SUWASA YATOA ELIMU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Posted on: Jul 18, 2025 Imetengenezwa: Jul 18, 2025
The Singida Urban Water and Sanitation Authority (SUWASA) has provided environmental conservation education to residents and business owners surrounding the Utemini clean water source.
The education, delivered by Environmental Engineer Kassim Mhehe and Public Relations and Communications Officer Neema Lulandala, focused on the harmful effects of dumping plastic waste near the water source.
Plastic waste causes significant environmental pollution due to its non-biodegradable nature and long-term persistence on the ground. As these plastics break down, they release chemicals that can seep into the soil and contaminate the water, which leads to high treatment costs for the Authority.
Furthermore, the accumulation of such waste on the ground creates breeding grounds for insects like mosquitoes, which can lead to diseases such as malaria and cholera—posing serious public health risks.
Residents were advised to store their waste in bags and load them onto municipal collection trucks. Strict action will be taken against anyone found dumping waste in the water source area.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imetoa elimu ya uhifadhi wa Mazingira kwa wakazi na wafanyabiashara wanaozunguka eneo la Chanzo cha Majisafi cha Utemini. Elimu hiyo iliyotolewa na Mhandisi Mazingira Kassim Mhehe na Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Neema Lulandala imeeleza madhara ya kutupa taka aina ya plastiki katika eneo la chanzo cha maji. Taka hizo aina ya plastiki husababisha uchafuzi mkubwa wa Mazingira kutokana na kutooza, kukaa juu ya ardhi kwa muda mrefu. Taka hizi zinapovunyikavunjika hutoa kemikali ambazo huweza kupenya chini ya ardhi na kuingia katika maji na kuchafua maji, ambapo huigharimu mamlaka fedha nyingi kuyatibu. Halikadhalika mlundikano wa taka hizo juu ya ardhi, husababisha mazalia ya wadudu kama mbu na wengineo, ambao husababisha magonjwa ya maralia na kipindupindu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu. Wakazi wa eneo hilo wameshauriwa kuhifadhi taka katika mifuko na kuzipakia katika Magari ya Manispaa, yanayopita kukusanya taka, Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekutwa akitupa taka latika eneo la chanzo cha maji.