MENEJIMENTI YA SUWASA YAKAA KIKAO NA MZABUNI KUTOKA PICOVOLT COMPANY LIMITED
Menejimenti ya Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira singida (SUWASA) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mha. Ramadhani Mtindasi leo tarehe 17.06.2027 imekaa kikao na Mzabuni kutoka "Picovolt Company Limited" Bw. Ogavian Ndago.
Lengo la kikao hicho ni kumtaka mzabuni huyo Kutekeleza kwa uharaka Majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusuppy pump mbili za Kisima Cha Utemini na Uhasibu .
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amemueleza mzabuni kuwa mara baada ya kumaliza Kusupply Pump ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia ukataba wa utekelezaji mradi huu unategemewa kukamilika Julai 25, 2026, Mkandarasi ameshauriwa kuanza utaratibu wa kuomba nyongeza ya muda wa utekelezaji wa mradi taratibu zitafuatwa kuona kama anastahili kuongezewa muda kulingana na sababu ziatakazo tolewa kuweza kukamilisha kazi hiyo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Mha. Ramadhani Mtindasi ameitaka timu yote ya Ufundi kuhakikisha inafanya kazi zote zilizosalia haraka iwezekanavyo ili kukamilisha visima hivyo viwili Kwani vikikamilika vitaongeza uzalishaji wa Maji na kupunguza shida ya Maji katika maeneo yenye shida na kupunguza Mgao Mkali wa Maji kwa maeneo yenye Mgao wa Maji.
##kazinaututunasongambele.