Habari
News
WARIOBA CONGRATULATES THE CREATIVITY OF SINGIDA WATER INSTITUTE STUDENTS
WARIOBA APONGEZA UBUNIFU WA WANAFUNZI CHUO CHA MAJI SINGIDA
Posted on: Jun 3, 2025 Imetengenezwa: Jun 3, 2025
The Managing Director of the Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) Sebastian Warioba has congratulated the students of Singida Water Institute, for their innovative work that is expected to help improve the work in the water sector in general. Warioba, who was the Guest of Honour at the 1st Innovation Exhibition for Singida Campus, held at the College, has congratulated the Students for demonstrating their creativity in using various methods to treat water, improve water supply, harvest rainwater, treat sewage and purify Dirty water originating from natural wells and ponds. Speaking to the students, he commended the good work being done by the Water College Management and the students they showed, as well as the good cooperation between SUWASA and the Water Institute. He has also encouraged them to develop such creativity so that it can be used to solve various challenges facing the water sector. He also advised the students to visit the SUWASA Waste Water Project area at Manga, to learn more. Singida Campus Manager Eng. Stephano Alphayo said the aim of the Exhibition is to help students apply the knowledge they have gained, in a work environment, show various stakeholders the work being done by the water college and enable this innovations to be used in improving service delivery in the Water Sector.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Sebastian Warioba amewapongeza wanafunzi wa Chuo cha Maji Kampasi ya Singida kwa Ubunifu wa kazi mbalimbali ambazo zinatarajiwa kusaidia kuboresha kazi katika Sekta ya maji kwa Ujumla.
Warioba ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Maonyesho ya 1 ya Ubunifu ya Chuo cha Maji kampasi ya Singida, yaliyofanyika eneo la Chuo hicho, tarehe 30/05/2025, ametoa Pongezi kwa Wanafunzi wa Chuo cha Maji kwa kuonyesha ubunifu wa kutumia mbinu mbalimbali Kutibu maji, kuboresha usambazaji maji, uvunaji wa maji ya mvua, kutibu majitaka pamoja na usafishaji wa maji machafu yanayotokana na visima vya asili na madimbwi.
Akiongea na Wanafunzi hao amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Chuo cha maji na wanafunzi waliyoionyesha, pamoja na ushirikiano mzuri kati ya SUWASA na Chuo cha Maji. Aidha amewahimiza kuendeleza ubunifu huo uweze kutumika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya maji. Pia amewashauri wanafunzi hao kufika katika eneo la mradi wa SUWASA wa Majitaka Manga kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Meneja Kampasi ya Singida Mha. Stephano Alphayo amesema lengo la Maonyesho hayo ni Kuwasaidia wanafunzi kutumia elimu waliyopata katika mazingira ya kazi, kuonyesha wadau mbalimbali kazi zinazofanywa na chuo cha maji na kuwezesha ubunifu huu kutumika katika kuboresha utoaji wa huduma Sekta ya Maji.