Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA SINGIDA ATEMBELEA KANDA YA IKUNGI/PUMA KUJUA HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo tarehe 02.07.2026 akiongozana na watumishi walio chini yake ametembelea Kanda ya SUWASA Ikungi/Puma ambayo pia ni sehemu ya eneo la huduma la SUWASA.
Katika ziara hiyo Mha. Ramadhani Mtindasi ametembelea Matanki ya Kuhifadhia maji yaliyopo Ulyampiti, Kitunguru, Halmashauri, Isunja na Ikungi pamoja na vyanzo vya maji vya maji vya Ikungi, Ighuka, Ulyampiti, Rafiki, Ikungi na Puma.
Lengo la ziara hiyo ni kuangalia hali ya mazingira ya vyanzo hivyo na uwezo wake wa sasa katika uzalishaji maji, ziara hiyo pia ilikuwa ina angalia namna nzuri ya kuboresha vyanzo hivyo na kuongeza uzalishaji lakini pia kuona namna ya kuchimba visima vingine na kuweza kupunguza nakisi iliyo kati ya uzalishaji na mahitaji. Kwa sasa SUWASA Ikungi/Puma inauwezo wa kuzalisha maji na kuweza kuhudumia asilimia 50 ya mahitaji.
Aidha Mkurugenzi Mtindasi amepokea taarifa ya utendaji kazi wa Kanda kutoka kwa Meneja wa SUWASA Kanda ya Ikungi/Puma Bw. James Malima ikiwepo miongoni mwa taarifa iliyo tolewa ni ya upungufu wa maji unaotokana kushuka kwa uzalishaji wa maji wa baadhi ya visima katika Kanda hiyo na kusababisha kuwepo na mgao wa maji kwa wateja pia Meneja Malima alizungumzia changamoto ya kanda hiyo kukabiliwa kuwa na mtandao mdogo wa mabomba ya Usambazaji. Mhandisi Mtindasi ameahidi kufanyia kazi changamoto hizo kwa kushirikiana na Menejimenti yake na kuweza kuboresha huduma ya MajiSafi katika Kanda hiyo kutoka asilimia 50 ya sasa na kufikia lengo lililo wekwa na Serikali la utoaji huduma ya maji mijini na vijijini.
Pia Mha. Ramadhani Mtindasi alipata nafasi ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwaajili ya kujitambulisha kama Mkurugenzi mpya wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Singida ili kuweza kumfahamu na kumpa ushirikiano katika kuwahudumia wananchi wa Ikungi/Puma.