WARNING: WATER METER THEFT – A REWARD OF 500,000 SHILLINGS WILL BE GIVEN TO ANYONE WHO IDENTIFIES THE CULPRITS.
TAHADHARI WIZI WA MITA ZA MAJI ZAWADI YA SHILINGI 500000 KUTOLEWA KWA ATAKAYEWABAINI
Content | Attachment |
---|---|
Maelezo | Kiambatanisho |
The Singida Water Supply and Sanitation Authority (SUWASA) issues a strong warning to citizens who are involved in the theft of water infrastructure, including water meters, taps, and other equipment related to water distribution. These acts are criminal offenses and a violation of the law, as such equipment is government property. Anyone found damaging or possessing this equipment without legal authorization will face strict legal action, including arrest and prosecution. Additionally, SUWASA warns scrap metal dealers and artisans who use these materials to make decorations or household items. Engaging in such activities constitutes participation in a criminal chain and is a punishable offense. All citizens are encouraged to report to the relevant authorities whenever they witness any person involved in the theft or destruction of water infrastructure. Anyone who provides accurate information leading to the arrest of water infrastructure thieves will receive a reward of TSh 500,000/=. LET US WORK TOGETHER TO PROTECT OUR INFRASTRUCTURE – WATER IS LIFE. Issued by: For more information, call toll-free: 0800710038 |
Download Attachment |
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) inatoa onyo kali kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa miundombinu ya maji ikiwemo mita za maji, koki na vifaa vingine vinavyohusiana na usambazaji wa maji. Vitendo hivyo ni vya kihalifu na ni uvunjaji wa sheria, kwani vifaa hivyo ni nyara za Serikali. Mtu yeyote atakayekutwa akiharibu au kumiliki vifaa hivyo bila ruhusa kisheria, atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Aidha, SUWASA inatoa onyo kwa wauza vyuma chakavu na mafundi wanaotengeneza mapambo au vifaa vya matumizi ya nyumbani kwa kutumia nyara hizi. Kufanya hivyo ni kushiriki katika mnyororo wa uhalifu, na ni kosa la jinai. Wananchi wote wanahimizwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapoona mtu yeyote akijihusisha na wizi au uharibifu wa miundombinu ya maji. Atakayefanikisha kutoa taarifa sahihi itakayopelekea kukamatwa kwa wezi wa miundombinu ya maji atajipatia zawadi ya shilingi 500,000/= TUSHIRIKIANE KULINDA MIUNDOMBINU YETU – MAJI NI UHAI. Imetolewa na: Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano wa Umma SUWASA 26/07/2025 Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0800710038 bure |
Pakua Kiambatisho |